Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ukuaji wa Zanzibar na ustawi wa siku zijazo unategemea uwekezaji, biashara, uchumi wa buluu na utalii.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipomkaribisha Rais wa Romania, Klaus Lohannis na Kampuni za nchini hiyo kufanya kazi pamoja katika masuala ya biashara, uwekezaji, uchumi wa buluu, utalii na sekta nyinginezo zenye maslahi kwa maendeleo.

Awali Rais huyo wa Romania alisema Romania itaendeleza ushirikiano ikiwemo kujumuisha kampuni zake kuanzisha biashara mpya Zanzibar, kukuza utalii, uchumi wa buluu, uwekezaji, pamoja na mabadilishano ya utamaduni na usimamizi wa urithi.

Leo, Novemba 19, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagana rasmi na Rais wa Romania, Klaus Werner Iohannis Viwanja vya Ikulu – Dar es Salaam ambaye amerejea nyumbani.

CCM wahimiza kusomesha Watoto manufaa fursa za uwekezaji - Mlao
Jokate awatembelea Wanafunzi wanaonyonyesha