Hatimaye sosholaiti kutoka Uganda, Zarinah Hassan ameondoka katika nyumba aliyokabidhiwa na aliyewahi kuwa mpenzi wake na mwanamuziki Diamond Platnumz nchini Afrika Kusini kama zawadi kwenye siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akitimiza miaka 36.

Hapo awali mama huyo wa watoto watano alikataa kuondoka katika kasri hilo, mali ya Diamond hata baada ya mashabiki wa msanii huyo kumtaka afanye hivyo na kudai kuwa nyumba hiyo si yake bali ya watoto wake ambao alizaa nae, Nillan pamoja na Tiffah.

Katika moja ya mahojiano aliyofanya Zari Afrika Kusini na moja ya Chombo cha habari hapa nchini kilichofunga safari hadi huko Zari alisikika akisema.

” Watu wakome kusema nyumba hiyo ni ya Diamond, nyumba hiyo ni ya watoto wangu ikizingatiwa kuwa mambo hayako shwari kati yangu na baba yao, wanapaswa kuwa na kitu watakachojivunia usoni na waseme wanakimiliki,” amesema Zari.

Kwa wiki kadhaa Zari amekuwa akirusha video mtandaoni za nyumba yake mpya, iliyokuwa ikifanyiwa nakshi za mwisho kabla ya kuhamia hapo na familia yake.

Zari kwa majivuno na ufahari mwingi alionyesha jinsi kasri hilo lilivyo zuri na tayari kuhamiwa na familia yake.

“Sasa nasubiri vitambaa vya madirishani. Navunja laana za tangu jadi,” Zari aliandika katika moja ya video hizo.

Aidha, Zari aliachana na Diamond Platinumz mwaka wa 2018 na imeripotiwa kuwa yuko na mpenzi ambaye wapo mbioni kufunga harusi na tayari mipango ya ndoa yao ipo jikoni.

 

Polisi yanasa wahamiaji haramu na nyara za Serikali
Prof. Kabudi ataja changamoto zinazoikabili Dunia