Mashabiki wa Diamond na Zari ambao tayari wamekuwa mashabiki wakubwa wa mtoto wa mastaa hao, Tiffah Naseeb, watarajie kuiona sura ya mtoto huyo.

Zari na Diamond Platinumz wamekuwa wakificha sura ya mtoto wao Tiffah katika mitandao ya kijamii kwa sababu ambazo zinaonekana kufanana na zile walizokuwa nazo mastaa wengine kama Beyonce na Jay Z, Kanye West na Kim Kardashian na kwa Afrika, Tiwa Savage na Tee Billz.

Mrembo huyo wa Uganda amejibu swali la mashabiki wao kwa ujumla wakati anajibu swali la shabiki mmoja aliyetaka kufahamu ‘ni lini wataionesha sura ya mtoto wao huyo wa kike’.

“Haudhani kama ni muda sasa wa kuonesha mashabiki wako sura ya mwanao Tiffah?” aliuliza shabiki huy. “Baada ya siku 40,” alijibu Zari.

Zarina

Zari pia alitumia maneno machache ya Kiganda kujibu tuhuma za King Lawrence aliyetaka wamfanyie Tiffah vipimo vya DNA, “Oyo Mulalu” akimaanisha “huyo niNi Kichaa”.

Stars Kuondoka Nchini Jumamosi
Oliseh Ambwaga Obi Na Victor Moses