Ikiwa ni siku moja toka msanii wa muziki Diamond Platinumz kutamka wazi kumsaliti mpenzi wake Zarina Hassan na kuchepuka na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond amefunguka na kujibu maoni mbalimbali ya watu waliotuma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kupitia akaunti yake ya Instagram.

Ambapo Zari amesimama kama mwanamke shupavu asiyerudishwa nyuma wala kukatishwa tamaa na matatizo yaliyotokea, kupitia tukio hilo ametoa faraja na ushauri kwa waliosalitiwa.

Ambapo amesema kuwaa amesikia masikitiko ya watu, ushauri na faraja na ameona jinsi ambavyo mashabiki wake wameumizwa na usaliti uliofanywa na baba watoto wake Diamond.

Hivyo amewaomba mashabiki hao wasilichukulie jambo hilo vibaya, wachukulie kama ni jambo jema kwani anaamini kuwa mtu akiamua kudanga sio kwamba anakudanganya wewe bali anajidanganya yeye na nafsi yake.

‘When a person chooses to cheat on you it’s not YOU actually it’s THEM which usually turns out that played themselves while they thought they are playing you’. Ameandika Zari

Amewaasa kuwa kikubwa ni kuzuia kujilaumu na kujifikiria una mapungufu kutokana na makosa ya mtu mwingine amesema kamwe usijilaumu, siku zote angalia jinsi gani utajiinua na kufanya maisha yaendelee.

You should never look down on yourself , don’t ever think you are worthless because of another persons mistakes and never blame yourself. But always look at how to pick yourself up and get ging.

Aidha amewataka mashabiki wake kuachana na mawazo mabaya juu ya jambo lililotokea na kushukuru kwa kila jambo kwani hivi karibuni aanakaribia kusherekea siku yake ya kuzaliwa.

 

Mpina: Serikali haitawavumilia wawekezaji
Video: Messi apiga nne Barcelona ikiibamiza Eibar 6-1