Kadri ambavyo tarehe za kupiga kura zinavyokaribia, suala lolote linalohusiana na siasa linapaswa kuchukuliwa kwa umakini sana hususan katika matukio yasiyo na uhusiano na siasa, la sivyo mambo yanaweza kuharibika.

Huko Mbeya, nusura ‘kitchen party’ iliyowakusanya wanawake zaidi ya 200 igeuka mpambano wa kisiasa baada ya dada wa bibi harusi mtarajiwa kutoa zawadi ya khanga na vitenge yenye rangi ya kijani na picha ya Magufuli kwa ajili ya kamati ya maandaalizi ya shughuli hiyo.

Ripoti kutoka jijini humo zinaeleza kuwa baada ya khanga  na vitenge hivyo kukabidhiwa kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, mmoja kati ya waalikwa aliifuata khanga moja na kuionesha kwa waalikwa huku akishangilia.

Haikuchukua sekunde kadhaa, baadhi ya waalikwa waliinuka na kutoka mbele huku wakionesha vidole viwili juu wakipaza sauti zao, “Tunataka Mabadiliko”.

Shukurani za pekee ziende kwa Brandy Nelson, mwandishi wa Mwananchi kwa ripoti hii.

Zaidi Ya Milioni 900 Zalipwa Kwa Kazi ‘Hewa’ Za Kandarasi
Fabio Capello: Tatizo Ni Mourinho Sio Wachezaji