Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC imewaengua wagombea 15 wa uwakilishi na saba wa udiwani kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kukiuka masharti ya ujazaji fomu za uteuzi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ZEC Thabiti Idarous Faina wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maamuzi ya rufaa za uteuzi wa wagombea wa uwakilishi na udiwani.

Mkurugenzi Faina amesema hawakufuata kanuni za uchaguzi kwenye zoezi la ujazaji fomu, wagombea kudhaminiwa na watu waliodhamini wagombea wengine.

Ameongeza kuwa makosa mengine ni baadhi ya wagobea waliokuwa watumishi wa umma kukiuka sheria za utumishi wa umma kugombea pasipo kuomba ruhusa ya waajiri wao kwa mujibu wa sheria.

Aidha amewataka wagoMbea waloteuliwa na ZEC kugombea kufuata sheria na kanuni za uchaguzi wakati wa kampeni ili kuepusha vitendo vya uvunjfu wa amani.

Facebook yadaiwa kuwafuatilia watumiaji wa Instagram
Yanga kama inanawa vile