Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ameituhumu Urusi kufanya ugaidi na mauaji ya raia kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na nchi hiyo katika miji kadhaa ya Ukraine hii leo Jumanne (Oktoba 18, 2022).

Zelensky, amesema mtu mmoja aliuwawa katika shambulizi la kombora lililofanywa dhidi ya jengo moja la makazi ya watu katika mji wa kusini wa Mykolaiv, ingawa hakutoa maelezo mengine zaidi ya waliouwawa licha ya ripoti za vifo vya watu saba katika tukio hilo.

Moja kati ya mashambuli katika vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Picha: The Indian Express.

Kupitia ujumbne wake, aliouandika kwenye mtandao wa Telegram, rais Zelensky amesema nchi yake iko katika mashambulizi yanayofanywa na wavamizi, na kusema watashambuliwa lakini hawatodhohofishwa kamwe.

Hata hivyo, taarifa nyingine zimeeleza kuwa mji wa Zhytomyr ulioko kaskazini mwa nchi ya Ukraine hauna huduma za maji wala umeme baada ya mashambulizi ya Urusi yaliyofanyika hii leo asubuhi (Oktoba 18, 2022).

Serikali kupelekea miundombinu ya mawasiliano DRC
Mgomo waanza nchi nzima kudai nyongeza ya mishahara