Uongozi wa Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar *ZFF* umekanusha taarifa za visiwa hivyo kupokwa uanachama ndani ya Shirikisho la soka Barani Afrika CAF.

Tangu juma lililopita Zanzibar imekua ikisemwa vibaya kuhusu kupokwa uanachama shirikishi wa CAF,  licha ya Shirikisho hilo la Afrika kutokutoa taarifa yoyote hadi sasa.

Meneja wa leseni za vilabu wa Shirikisho la soka visiwani Zanzibar *ZFF*, Mbarouk Suleiman Othman, amesema mpaka kufikia leo Jumatano, (Julai 14, 2021), vilabu vya KMKM na Mafunzo ndiyo Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho kwa msimu ujao 2021-22.

Amesema taarifa za Zanzibar kupokwa uanachama shirikishi ni uvumi wa kujipatia umaarufu mitandaoni na kwamba CAF wana utaratibu rasmi wa kuwasiliana na nchi wanachama.

Tanzania imekua na nafasi ya kipee ya uwakilishi kwenye michuano ya vilabu, kwa kushirikisha timu mbili zaidi kutoka Zanzibar.

Msimu ujao Tanzania Bara itawakilishwa na timu nne kwenye michuano ya vilabu barani Afrika.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 15, 2021
Waziri Junior atema nyongo, ukame wa mabao wamuhuzunisha