Meneja wa mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid Zinedine Zidane amemwagia sifa mshambuliaji kutoka Ufaransa Karim Benzema, kwa kusema mchezaji huyo ana ubora wa kipekee.

Zidane alimwaga sifa hizo kwa Benzema, kufautia kufanikisha mpango wa kuiwezesha Real Madrid kuibuka na ushidni wa mabao matatu kwa moja dhidi ya kwenye mchezo wa Ligi ya Hispania dhidi ya Athetic Bilbao, uliochezwa usiku wa kuamkia leo Jumatano (Desemba 16).

Kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, Benzema alifunga mabao mawili, miongoni mwa mabao matatu yaliyoiwezesha Real Madrid kufikisha alama sawa dhidi ya Real Sociedad na Atletico kwenye msimamo wa Ligi ya Hispania (La Liga).

Zidane amesema Benzema amekua msaada mkubwa kwenye kikosi chake, na siku zote humfanyia tathmini na kujiridhisha wazi kuwa ni mshambuliaji mwenye ubora na kiwango cha kipekee.

Amesema hajawahi kumuona mchezaji kama Benzema katika miaka ya hivi karibuni, hasa ikizingatiwa safu ya ushambulaiji wa mabingwa hao wa Hispania imekua ikimtazama kama muokozi.

“Kwangu Ndiyo, kwa kuongeza kwa anachokifanya, anachokionyesha, amekuwepo Real Madrid kwa muda mrefu.”

“Amecheza zaidi ya Michezo 500, mabao yote, rekodi zake. Alichokifanya kinajieleza chenyewe. Kwangu ni bora, ipo wazi kabisa.” Amesema Zidane.

Mabao mawili aliyofunga dhidi ya Athetic Bilbao, yanamuwezesha Benzema kufikisha idadi ya mabao 10 aliofunga kwenye michuano yote msimu huu, ikiwa ni zaidi ya mchezaji yeyote wa ligi ya Hispania (La Liga).

Uganda: Tume ya mawasiliano yaitaka google kufunga vituo hivi Youtube
Wasiwasi watanda idadi kubwa ya watu kukosa chanjo ya Corona

Comments

comments