Remix ya wimbo AY ‘Zigo’, ulioshambuliwa vyema na msanii huyo pamoja na Diamond Platinumz chini ya watayarishaji watatu, Nahreel, Hermy B na Marco Chali umeingia kwenye reko kubwa duniani.

Wimbo huo uliotoa wiki hii pamoja na video yake, umeweza kusikilizwa zaidi ya mara 14,000 kwa siku moja kati ya nyimbo 10 duniani zilizosikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Audiomack.

Wimbo huo sasa unapigana vikumbo na nyimbo nyingine 9 za wasanii wakubwa duniani akiwemo Akon, Wiz Khalifa, Tyga, Meek Mill na wengine.

 

Ali Kiba aonesha Upendo kwa Diamond kwa njia hii
Mwenyekiti wa ZEC, Jecha atangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi Zanzibar