Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, anakabiliwa na mtihani mgumu katika umeneja wake wakati atakapokutana na Liverpool siku ya Jumapili, huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa na wasiwasi wa kutofuzu kucheza Champons League (Times).

Wadhamini wa Manchester United, Adidas wanataka mshambuliaji wa Barcelona, Messi, kuungana na Pep Guardiola Old Trafford, meneja huyo atakapomaliza muda wake Bayern Munich (Marca).

Meneja wa Paris St-Germain, Laurent Blanc anasema tabia ya mshambuliaji Edinson Cavani imekuwa “tatizo” na yuko tayari kumuacha aondoke mchezaji huyo kutoka Uruguay (Daily Mail)

Chelsea wamepanda dau la pauni milioni 40 kumtaka kiungo wa Real Madrid, Mjerumani Toni Kroos, ambaye pia amehusishwa na Liverpool na Manchester United (Fichajes)

Chelsea pia wanapambana na Inter Milan na Barcelona kumsajili mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi (Daily Mirror).

Liverpool wamekubaliana na Schalke, kumsajili bila malipo yoyote beki wa kati Joel Matip mwisho wa msimu (Daily Mirror)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Matthias Sammer hajasema waziwazi iwapo Mario Gotze, ambaye anasakwa na Liverpool, atasalia Bayern (Daily Express)

Manchester United wanakaribia kumsajili beki wa kati kutoka Austria, Aleksandar Dragovic, anayeichezea Dynamo Kiev kwa pauni milioni 16 (Sport Mediaset)

Mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, huenda akalazimika kubakia na timu hiyo baada ya Tottenham kutokuwa tayari kulipa pauni milioni 23 walizotaka kutoa msimu uliopita, huku meneja Mauricio Pochettino akiwa hana uhakika kama ni mchezaji anayemtaka (Sun), hata hivyo Stoke City wanamtaka Berahino (Times)

Mshambuliaji wa Charlton, Ademola Lookman, 18, anasakwa na Manchester City, Chelsea, Everton na Tottenham (Independent).

Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, ametakiwa kufika mahakamani kuhusiana na sakata la uhamisho wake kutoka Santos mwaka 2013 (Guardian)

Meneja wa Aston Villa, Remi Garde ana matumaini ya kumsajili beki kutoka Senegal, Lamine Sane kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, akitokea Bordeaux (Telegraph)

Beki wa kushoto kutoka Ghana Baba Rahman anaanza kughadhibika kutokana na kutopangwa kwenye kikosi cha Chelsea, tangu alipohamia akitokea Augsburg (Bild)

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal anamtaka mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Islam Slimani kwa pauni milioni 12 (Sun).

Penzi la Mrembo huyu lilikuwa chambo ya kumkamata Bilionea wa Unga 'El Chapo', Meseji zao ziko hapa
Laurent Blanc Athibitisha Bifu Lake Na Cavani