Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Pwani, kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo WMA wametoa elimu ya kujilinda moto na jinsi ya kuhakiki ujazo wa gasi kwa wauza mitungi ya gesi Wilayani Kibaha, ili kuwalinda na athari za moto na Wananchi kupata ujazo unaowiana na pesa waliyolipa.

Akitoa mada kwenye Kongamano la mwaka la Wafanyabishara wa uzalilishaji wa mitungi ya gesi mjini Kibaha Pwani, Afisa Wakala wa Vipimo WMA Mkoa wa Pwani, Isaack Bilahi amesema kutoa elimu ya uhakiki ujazo wa mitungi ya gasi kwa wauza wa mitungi, ni kutimiza takwa la kisheria.

Amesema, lengo la Serikali kuagiza Wakala wa Vipimo WMA kusimamia upimaji wa mitungi ya gasi ni kumlinda Mteja apate gasi yenye ujazo na uzito sahihi na kuwataka wauzaji kuhakikisha wanapokea na kupima mitungi wanayoletewa na wauzaji wa jumla ili kupata uhakiki.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Pwani Surgent Banasani Janja amesema uvutaji wa sigara hautakiwi na katika ukaguzi watakaofanya watahakiki kama dkuna bango la “usivute sigara” na uwepo wa mitungi ya kuzima moto, “fire extinguisher”.

Naye Afisa Masoko wa ECO Africa, Abdullatif Jafar Abeid amewataka Watanzania kutumia vifaa vya kuunganisha jiko na mitungi ya gesi vyenye ubora, ili kudhibiti matukio ya moto na usalama wao ambavyo ni pamoja na mipira ya gasi, banner, majiko yenyewe na viberiti vyote kutoka ECO Africa ambavyo vina ubora na ni madhubuti.

CCM wahimizana kudumisha umoja, mshikamano
Kipindupindu: Mataifa yachukue tahadhari mapema - WHO