Matokeo ya awali ya kura za wabunge nchini Zimbabwe, yanaonesha kuwepo kwa mchuano mkali kati ya Chama Tawala na Chama Kikuu cha Upinzani siku ya Ijumaa.

Katika uchaguzi huo ambao Chama cha Rais Emmerson Mnangagwa (80), cha ZANU-PF, kilichokuwa madarakani kwa muda wa miaka 43, kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuendelea kubaki madarakani.

Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imesema bado inahakiki matokeo kutoka takriban vituo vya uchaguzi 12,500, na itaweza kuanza kutangaza matokeo siku ya Ijumaa. Matokeo ya kura za urais hayatarajiwi kutangazwa kwa siku kadhaa.

Zimbabwe ina historia ndefu ya uchaguzi wenye utata, kitu ambacho kinawafanya watu wengi kuwa na mashaka kuhusu matokeo rasmi ya uchaguzi huo huku nchi hiyo ikikabiliwa na mfumuko wa bei na ongezeko la ukosefu mkubwa wa ajira.

Thamani ya dola kibiashara Tanzania, China yaendelea kupaa
Serikali yataka vipaumbele fedha miradi ya Mazingira