Polisi nchini Zimbabwe wanasema wamewakamata watu 41, simu za mkononi, talakilishi na vifaa vingine vya kielektroniki wakati wa msako mkali katika maeneo manne ya jijini Harare mara baada ya kupata taarifa za uasi na uhalifu, wakati huu muhimu wa uchaguzi wa Kitaifa.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi nchini humo, Paul Nyathi amesema Vifaa hivyo, vinadaiwa vilikuwa vikitumika kujumlisha isivyo halali takwimu za upigaji kura na matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kote nchini,” alisema katika taarifa.

Aidha, Polisi pia imeyataja baadhi ya mashirika yaliyolengwa kuwa ni Mtandao wa kufuatillia uchaguzi wa Zimbabwe Support Network, Kituo cha Rasilimali za Uchaguzi na Team Pachedu – yote yakiwa ni makundi maarufu ya kiraia ambayo yalisema yanafuatilia uchaguzi huo kwa maslahi ya demokrasia.

Raia wa Zimbabwe walipigia kura ya Urais, Wabunge, na Madiwani siku ya Jumatano, huku wengi wakielezea matumaini ya mabadiliko baada ya miaka mingi ya matatizo ya kiuchumi. Lakini wachambuzi walionya kuwa haiwezekani chama tawala cha ZANU-PF kuachia madaraka ambayo kimeyashikilia kwa miaka 43.

Tayari, matokeo ya kwanza ya maeneo bunge yalitangazwa siku ya Alhamisi katika uchaguzi wa Zimbabwe baada ya zoezi hilo kucheleweshwa, na hata kuongewewa muda katika baadhi ya vitongoji, ikiwa ni chini ya maeneo 10 ya Bunge kati ya 210, ambayo yalikuwa yameangaza hadi hapo jana Alhamisi, Agosti 24, 2023.

Upinzani wa kisiasa nchini Zimbabwe na wachambuzi huru kwa muda mrefu wamekuwa wakiwashutumu polisi kwa kupenedelea upand mmoja, huku mikutano ya upinzani mara nyingi ikipigwa marufuku au kutawanywa, na watu wanaoikosoa serikali kukamatwa kiholela. Polisi wamekanusha madai ya upendeleo.

Ahmed Ally: Hatutaki kufungwa fungwa
Fluminense yaiwekea ngumu Liverpool