Timu ya Taifa ya Zimbabwe, ‘Zimbabwe Warriors’ imejiondoa kwenye mashindano ya CECAFA Challenge ambayo yamepangwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3,mwaka huu, nchini Kenya.

Zimbabwe ambayo ilikuwa ni timu mwalikwa kutoka nje ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, imeleeza kuwa imefikia uamuzi huo kutokana na sababu za kiusalama nchini Kenya, na ni baada ya kushauriana na wadau mbalimbali wa soka nchini humo (Zimbabwe).

Sehemu ya taarifa iliyotolewa na chama cha soka nchini Zimbabwe zimeeleza “ZIFA inasisitiza utayari wa mashindano yoyote yajayo ikiwa mazingira katika mashindano hayo, si hatarishi kwa timu shiriki. Kujitoa kwetu katika mashindano hayo muhimu ni pigo kwetu, kwa timu, kwa taifa na kwa waandaaji pia lakini ilibidi kufikia uamuzi huu kwa maslahi mapana ya washiriki wote”.

ZIFA imeomba radhi kwa waandaji, wadhamini, mashabiki wa soka pamoja na wadau mbalimbali kwa usumbufu huku ikikaribisha fursa ya mashindano kama hayo kutoka kwa CECAFA au vyama vingine vya soka kwa wakati mwingine.

Kujiondoa kwa Zimbabwe kunafanya timu shiriki sasa kubaki tisa badala ya kumi za awali.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 30, 2017
Maandalizi michezo ya mabunge Afrika Mashariki