Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amejibu tuhuma za kikosi chake kuhusishwa na mpango wa kubebwa na waamuzi kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Villareal.

Kiungo wa Villareal Bruno Soriano alimtuhumu mwamuzi wa mchezo huo, kwa kusema aliwabeba makusudi Real Madrid kwa kitendo chake cha kuwapa mkwaju wa Penati kwa kisingizio cha aliunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Bruno alidai jambo hilo lilifanywa kwa makusudi na mwamuzi huyo, baada ya mambo kuwaendelea kombo Real Madrid, ambapo ulishuhudia walikua nyuma kwa mabao mawili kabla ya kuanza kurudisha na kupata ushindi wa mabao matatu.

Zidane amesema hakuna ukweli wa jambo hilo, zaidi ya juhudi za wachezaji wake kupambana hadi dakika ya mwisho, na kupata matokeo ya kuridhisha.

Meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, amesema huenda Bruno Soriano alikuwa na mihemko ya hasira zilizotokana na kupoteza mchezo, na ndio maana akatumbukia katika shimo la kuituhumu Real Madrid kwa kuihusishwa na mwamuzi.

Wakati huo huo kikosi cha Real Madrid usiku wa kuamkia hii leo kilishindwa kufurukuta katika mchezo wa ligi ya Hispania, baada ya kulazimishwa sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Las Palmas.

Matokeo hayo yameishusha Real Madrid kileleni na sasa inashika nafasi ya pili, kufuatia wapinzani wao FC Barcelona kushinda mchezo wao dhidi ya Sporting Gijon ambao wamekubali kichapo cha mabao sita kwa moja.

FC Barcelona wamefikisha point 57 wakiizidi point moja Real Madrid ambayo bado ina faida ya mchezo mmoja mkononi.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya Hispania iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Osasuna 1 – 4 Villarreal

Celta Vigo 2 – 2 Espanyol

Granada 2 – 1 Alaves

Video: LHRC kuendesha Kampeni ya Uhuru wa kujieleza
Fainali Za Kombe La Dunia 2018: Uingereza Yajishusha Kwa Urusi