Baada ya kukamilika kwa msimu wa 2019/20, Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza orodha ya klabu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao wa 2020/21.

TFF wametangaza orodha hiyo baada ya kukamilika kwa michezo ya mtoano, iliyohusisha klabu mbili za Ligi Daraja la Kwanza na klabu mbili kutoka Ligi Kuu (VPL) msimu wa 2019/20.

Klabu kutoka ligi Daraja la Kwanza zilizocheza hatua hiyo zilikua Geita Gold SC na Ihefu FC huku zile za Ligi Kuu ni Mbeya City FC na Mbao FC.

Michezo ya mkondo wa pili iliyochezwa mwishoni mwa juma lililopita iliamua timu za Mbao FC na Geita Gold SC kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao, huku Ihefu FC na Mbeya City FC zikiwa miongoni mwa klabu zitakazocheza Ligi Kuu (VPL).

Orodha ya timu zitakazoshiriki ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2020/21.

Timu 20 ambazo zitacheza ligi Daraja la kwanza msimu 2020/21

Timu 12 zilizobaki ligi Daraja la kwanza

1-Majimaji FC (Ruvuma)

2-Mbeya Kwanza (Mbeya)

3-Njombe Mji (Njombe)

4-African Lyon (Dar)

5-Boma FC (Mbeya)

6-Geita Gold FC (Geita)

7-Transit Camp (Dar)

8-Gipco FC (Geita)

9-Arusha FC (Arusha)

10-Rhino Rangers (Tabora)

11-Mawenzi Market (Morogoro)

12-Pamba SC (Mwanza)

Timu 5 ilizoshuka Daraja kutoka ligi kuu

1-Singida United (Singida)

2-Ndanda FC (Mtwara)

3-Lipuli FC (Iringa)

4-Alliance FC (Mwanza)

5-Mbao FC (Mwanza)

Timu 3 Zilizopanda FDL kutoka ligi Daraja la Pili (SDL)

1-Fountain Gate FC (Dodoma)

2-Kitayosce (Tabora)

3-African Sports (Tanga)

Waziri Kairuki atembelea maonesho ya Nanenane, akumbusha zabuni kwa makundi maalum
Infantino kuendelea na kazi FIFA