Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, amempongeza Rais John Magufuli kwa kukabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika jana Mjini Dodoma.

Magufuli na Kikwete Uenyekiti

Zitto amepongeza utaratibu wa CCM kukabidhiana uongozi kila baada ya muda, jambo ambalo amesema ni muhimu kwa vyama vingine vya siasa barani Afrika kujifunza.

Kadhalika, Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini alieleza matarajio yake kwa Rais Magufuli kuona umuhimu wa kufanya siasa kwa mujibu wa sheria.

“Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu. Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais,” Zitto ameandika kupitia akaunti yake ya Facebook.

Hivi karibuni, Zitto alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliokumbwa na rungu la dola akihojiwa kwa kukaidi agizo la Serikali la kutofanya mikutano.

 

Terence Crawford amdunda Viktor Postol
Magufuli aeleza ambacho angewafanya CCM kwa kumuimbia Lowassa