Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ameonekana kutofurahishwa na uamuzi wa Rais Magufuli kusamehe wafungwa ambao ni wanamuziki mashuhuri, Nguza Viking (Babu Seya) na mwanaye ‘Papii Kocha’.

Tangu utangazwe msamaha huo, na Rais Dkt. Magufuli, Zitto amekuwa akiandika na kutoa kauli zinazoonyesha kupingana na jambo hilo licha ya Rais kuwa na mamlaka kikatiba kumsamehe mfungwa yeyote akiona inafaa.

“Waliozomea na kuzodoa ahadi ile walikuwa sahihi. Wanaomzomea Rais kwa kutoa msamaha wapo sahihi pia. Hakuna sababu kuzodoana. Tukemee wabakaji kusamehewa kiholela,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Lissu afunguka tena jijini Nairobi
Nchi za Kiarabu zataka kufutwa kwa maamuzi ya Trump