Kufuatia matukio yanayoendelea Afrika hasa katika ngazi ya Serikali, mambo mengi yameibuka ambayo hayaleti picha nzuri miongoni mwa Afrika na dunia kwa ujumla.
Kupitia kurasa wa Twitter na facebook Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ametoa hoja iliyoibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii.
Amesema ”Kuna upepo mkali wa mabadiliko Afrika. Jana na leo Viongozi wa Mataifa makubwa Afrika wameachia ngazi. Zuma Afrika Kusini na Haile Mariam Desalegn wa Ethiopia naye kaachia ngazi mchana huu”.
Kumekuwa na ushindani mkubwa katika kung’ang’ania madaraka hali ambayo imeleta kutoweka kwa demokrasia na matumizi ya mabavu kuhusika.
Hivi karibuni nchini Kenya kumetokea mtafuruko mkubwa katika uchaguzi wa Urais, hali iyopelekea viongozi kuvunja katiba za nchi na kujichukulia sheria mkononi.
-
Video: Kamanda Musilimu kula sahani moja na waegesha magari
-
Makonda awashushia neema walimu
-
Video: Ramaphosa aapishwa kuwa Rais wa Afrika Kusini
Hali kadhalika nchini Afrika kusini, aliyekuwa Rais nchini humo, Jacob Zuma kajiuzulu kupitia nguvu ya chama hicho cha ANC, hali iliyopelekea aliyekuwa Mwenyekiti wa chama Tawala ANC, Cyril Ramaphosa kuteuliwa na kuapishwa kama Rais wa nchi hiyo.
Vivyo hivyo aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Ethiopia Hailemariam Desalegn amejiuzulu akidai amefanya hivyo ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.
Bila kusahau nchini Tanzani kuna mambo mengi sana kisiasa yanayoendelea ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina.
Je ni uroho wa madaraka na uminywaji wa demokrasia au ni katika harakati za kujenga uchumi wa nchi hivyo kuna baadhi ya mambo lazima yapatiwe ufumbuzi kufikia lengo la kujenga nchi imara kiuchumi.
Je kisiasa hii inaashiria nini, kama mdau toa maoni yako.