Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameungana na kauli ya wanazuoni kumuomba Rais John Magufuli kuamrisha mamlaka husika kumkamata mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP yenye mitambo ya kufua umeme iliyozua sakata la ESCROW, Harbinder Sing Sethi.

Uongozi wa Jumuiya ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA) hivi karibuni walimtaka Rais Magufuli kufanikisha utekelezaji wa azimio namba moja la Bunge kufuatia sakata la Escrow.

Azimio namba moja la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu hatua za kuwachukuliwa dhidi ya Sethi ambaye kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya PAC iliyokuwa chini ya uenyekitiwa wa Zitto Kabwe alisababishia taifa hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 320, ni kuchukuliwa hatua kwa kufanya jinai kwa kusababisha upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 320 za umma.

“Tunashangaa mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW hayajatekelezwa na badala yake wanaishia kuwatoa kafala akina William Ngeleja na Anna Tibaijuka. Hii haitakiwi kuiacha hivi hivi. Lazima sisi kama vijana wasomi tusimame kulitetea taifa letu na rasilimali zake,” Katibu wa JUWARA, Mahmubu Salibaba aliliambia Jamvi la Habari.

Nemanja Vidic Avunja Ukimya
Cesc Fabregas Amfukuzisha Kazi Mfanyakazi Wa Chelsea