Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amechoshwa na mambo yanayoendelea kuhusu Abdul Nondo na kuwaomba wazee wa Kigoma kuingilia kati.
Ameyasema hayo mara baada ya Idara ya Uhamiaji kumuhoji kuhusu uraia wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo jambo ambalo Zitto Kabwe amesema idara ya uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo.
“Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana ‘credentials’ ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo,”amesema Zitto Kabwe
Hata hivyo, Mwanafunzi Abdul Nondo aliitwa na Idara ya Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake na kujaza fomu hivyo anapaswa kufika tena ofisi za uhamiaji tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kupeleka vyeti vya kuzaliwa yeye, baba na mama yake, na bibi na babu kwa pande zote mbili za wazazi wake.
-
Serikali yamuomba Mdee kusaidia utatuzi mgogoro wa Ardhi
-
Nondo kuteta na IGP, DCI na AG Mahakamani
-
Msajili atakiwa kufuta vyama vya siasa ‘korofi’