Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe ametangaza rasmi uamuzi wa chama chake kutojiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu.

Akiwahutubia wanachama wa chama hicho jana (Julai 26), Zitto Kabwe alisema kuwa chama chake kimeamua rasmi kutojiunga na umoja huo kwa kuwa kinatofutiana na mfumo wa kanuni za vyama vingine. Hususan katika kutambua miiko ya maadili.

“Maamuzi yetu lazima yaendane na chama chetu kinapata nini. Sisi tuna mambo ambayo vyama vingine havina. Kwa mfano, sisi tuna Azimio la Tabora,” alisema.

“Azimio la Tabora sehemu ya nne inazungumzia miiko ya maadili ya viongozi. Kwamba kwanza ni lazima kiongozi wa kisiasa wa umma atangaze mali, madeni na maslahi yake,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, mwanachama wa chama hicho, Diana Simba alitangaza rasmi uamuzi wake wa kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho.

NATO Yaitisha Kikao Cha Dharura Kujadili ‘Mchezo Wa Vita’
Tanzia: Mtoto Wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Afariki