Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake jijini Dar es salaam  na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Taarifa fupi iliyotolewa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis, amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo huku akibainisha kwamba sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi katika kata ya Kijichi, Jijini Dar es salam.

Amesema kuwa katika hotuba yake aliyoitoa Kijichi jijini Dar es salaam, Zitto alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu masuala ya mwenendo wa uchumi wa Taifa unavyoyumba, hivyo inawezekana ikawa ni miongoni mwa sababu za kukamatwa kwake.

Mavunde awataka vijana kuchangamkia fursa
Hakuna ndoa kati ya Dogo janja na Irene Uwoya?