Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ameeleza kuridhishwa na mkakati wa rais John Magufuli hususan katika kupambana na ufisadi.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa watanzania wanapaswa kumuunga mkono rais Magufuli katika kupambana na ufisadi na juhudi zake za kurudisha viwanda nchini.

Ameeleza kuwa asilimia 60 ya masuala aliyoyaongelea Rais kwenye hotuba yake bungeni yamo kwenye ilani ya ACT – Wazalendo ambayo walimpa baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa urais.

“Nilipokuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge nilikuwa nikitoa taarifa mbalimbali kuhusu wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishwaji, sasa tumepata Rais anayetaka kupambana na ufisadi na kurudisha viwanda, tunapaswa kumuunga mkono. ”

 

Sheria mpya ya Usalama Bararani kuwanyoosha madereva 'kielekroniki'
Lowassa akwama Mwanza, Polisi wawazuia Chadema Kuuaga mwili wa Mawazo kuhofia kipindupindu