Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amewashukiwa wasanii wa Tanzania ambao wameonekana katika majukwaa ya siasa wakipigia debe chama fulani, akiwataka kutafakari kwa kina kwa kuwa wanatumiwa na kushuka thamani baada ya kampeni.

Zitto amedai kuwa wanasiasa hao ambao hivi sasa wanasema kuwa wanawapigania na kuwatetea wasanii hao si wa kweli kwa kuwa hawakufanya hivyo wakati wakiwa madarakani hata pale hoja hizo zilizopowekwa mezani.

“Wasanii wa Tanzania, wakati tunatetea kazi zenu kurasmishwa ili mfaidi jasho lenu, hawa mnaowaimbia Leo hawaikuinua mdomo wao kuwatetea. Kampeni zikiisha na thamani yenu imeisha. Tulipopaza sauti kupinga unyonyaji wa makampuni ya simu kwenye RBT hawa wanaoahidi kuwatetea Leo hata habari walikuwa hawana. Naomba mtafakari sana hatma ya tasnia yenu,” Zitto ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram.

Dk. Shein Amkana Maalim Seif, Adai ZEC Iko Sawa Na CCM Itashinda
Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Zamani Akamatwa Na Kulala Selo