Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ujumbe wake kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza kufuatia matokeo ya utafiti wa taasisi hiyo uliompa Dk Magufuli ushindi wa kishindo wa 65%.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Zitto amewataka Twaweza kufanya utafiti huo tena kwa madai kuwa utafiti huo ulifanywa kabla chama hicho hakijawa na mgombea urais na hakijafanya uzinduzi wa kampeni zake.

Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa chama chake kinaamini katika tafiti na kwamba kinayapokea matokeo ya aina yoyote, yawe hasi au chanya. ACT – Wazalendo imemsimamisha Bi. Anna Mghwira kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.

UTAFITI-TWAWEZA

Joto La Mpambano Wa Simba Na Yanga
Balotelli Achangia Ushindi Wa AC Milan