Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa vyama vya upinzani vinakusudia kwenda Mahakamani kufungua kesi dhidi ya serikali kwa kuwazuia kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa matawi ya chama hicho jijini Mwanza, ambapo ameongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa sheria ya vyama vya siasa haimtaji rais mahali popote kuwa ana mamlaka kisheria kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa

“Asiwadanganye mtu yeyote, awe na cheo chochote kwamba kuna nyakati za kufanya siasa na nyakati za kufanya mandeleo. Wakati wote ni wakati wa siasa na kufanya maendeo, kwa sababu siasa ni maendeleo, na sasa tumekubaliana tufungue kesi kuishtaki Serikali ili mahakama itoe ruhusa ya kuendelea na zetu za kisiasa,”amesema Zitto

Aidha, amesema kuwa uhuru wa kidemokrasia hivi sasa unaendelea kuminywa na kuwataka wananchi wasidanganywe kirahisi kuwa muda wa kufanya siasa umeisha, kwani wakati wote ni wakati wa siasa kwa sababu hata hayo maendeleo yanaletwa na siasa pia.

Hata hivyo, mwaka 2015 baada ya Rais Magufuli kuapishwa alizuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa, akisema kuwa wakati wa siasa umeisha hivyo ni muhimu wakaacha kushabikia siasa na kujikita kwenye shughuli za maendeleo zaidi.

Kylian Mbappe Kucheza Kwa Mwaka Mmoja PSG
Ozil: Wachezaji Tunapaswa Kulaumiwa