Zaidi ya watu 14 wamethibitishwa kufa maji katika ziwa Victoria baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama huko nchini Uganda.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili ya ovemba 25, 2018,  huku mashua hiyo ikiwa kwenye safari ya kutoka Port Bell Luzira kuelekea kisiwa cha Mutima.

Maafisa wa usalama wa nchini Uganda wamesema kwamba chanzo cha mashua hiyo kuzama ni uzito uliopitiliza, na mpaka sasa watu 40 wameshaokolewa.

Aidha, taarifa zaidi zimesema kuwa mashua hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya watu 100, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya vifo ikaongezeka.

Ajali za maji zinazosababisha vifo katika ziwa Victoria zimekuwa zikitokea mara kwa mara, ambapo hivi karibu Tanzania ilipoteza zaidi ya watu 200 kutokana na kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe.

 

Mwanri aainisha maeneo manne ya uwekezaji mkoa wa Tabora
Watanzania msitegemee kupata kirahisi kitambulisho cha taifa- Kangi Lugola