Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic ameweka rekodi mpya kwenye klabu ya Paris St-Germain, baada ya kufunga mabao mawili muhimu katika mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa dhidi ya Olympic Marseille hapo jana.

Zlatan alifunga mabao hayo kwa njia ya mikwaju ya penati, na kuipa ushindi PSG ambayo ilikua nyuma kwa bao moja kwa dakika 11, baada ya wapinzani wao kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 30 kupitia kwa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Michy Batshuayi Tunga.

Zlatan alifunga mabao hayo mawili katika dakika ya 41 na 44 na kufanikiwa kufikisha idadi ya mabao 110 tangu aliposajiliwa huko Parc des Prince, 17 Julai 2012.

Mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 34, amevunja rekodi ya ufungaji wa muda wote wa klabu hiyo kwa kuifikia ile iliyokua imewekwa na Pedro Miguel Pauleta aliyekua anaongoza kwa kufunga mabao 109, na sasa ameivuka kwa kufunga mabao 110.

Ushindi wa mabao mawili kwa moja uliopatikana jana, umeendelea kuiweka kileleni PSG kwa tofauti ya point tano katika msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa.

Harakati Za Kuelekea Urusi Mwaka 2018
Van Gaal Awatafutia Jina Wachezaji Wake