Mshambuliaji wa Man Utd Zlatan Ibrahimovic, ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi kupitia tovuti ya Eurosport kwa mwezi Agosti.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Sweden alipata kura nyingi zaidi ya wachezaji wengine ambao walikua anashindanishwa nao, kufuatia viwango walivyovionyesha katika mwezi Agosti ambapo ligi kadhaa za barani Ulaya zilianza kutimua vumbi.

Mashabiki 60,000 ulimwenguni walishiriki kupiga kura kupitia tovuti ya Eurosports ambayo imeanzisha mchakato huo katika kipindi hiki cha msimu wa 2016/17.

Upigaji wa kura hizo, umetathminiwa kwa alama (point) kwa kila mshiriki na mwisho wa shindano Ibrahimovich aliongoza kwa kupata alama 10, mbele ya mpinzani wake wa karibu Sami Khedira wa Juventus FC.

Orodha ya wachezaji walioshirikishwa kwa mwezi Agosti pamoja na matokeo ya kura zilizopiga.

  1. Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) – 10 points
  2. Sami Khedira (Juventus) – 9 points
  3. Layvin Kurzawa (Paris Saint-Germain) – 8 points
  4. Domenico Berardi (Sassuolo) – 7 points
  5. Alexanre Lacazette (Lyon) – 6 points
  6. Arda Turan (Barcelona) – 5 points
  7. Robert Lewandowski (Bayern Munich) – 4 points
  8. Marcos Asensio (Real Madrid) – 3 points
  9. Raheem Sterling (Manchester City) – 2 points
  10. Andre Schurrle (Borussia Dortmund) – 1 point

Mchakato wa kumpata mchezaji bora wa kila mwezi kupitia Eurosports, unashirikisha ligi tano kubwa barani Ulaya ambazo ni Premier League (England), La Liga (Hispania), Bundesliga (Ujerumani), Serie A (Italia), Ligue 1 (Ufaransa).

Picha: Waziri Mkuu awasili Dodoma kwaajili ya Bunge
Picha: Waziri Mkuu awasili Dodoma kwaajili ya Bunge