Meneja wa Man Utd, Jose Mourinho anatamuacha mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic, katika orodha ya wachezaji ambao atakwenda nao nchini China kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu wa 2016-17.

Man Utd wanatarajia kuondoka nchini England kuelekea China, siku ya jumanne ya juma lijalo.

Ibrahimovic bado yupo katika mapumziko baada ya fainali za Euro 2016 ambazo zilifanyika nchini Ufaransa na huenda akajiunga na wenzake juma moja lijalo.

Wachezaji wengine ambao hawatokuwa sehemu ya kikosi cha Man Utd ambacho kitasafiari kuelekea mashariki ya mbali ni Wayne Rooney, Chris Smalling pamoja na Marcus Rashford.

Kikosi cha Man Utd kitakachofanya safari ya nchini China kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund mjini Shanghai Julai 22 na kicha Manchester City mchezo ambao umepangwa kuunguruma mjini Beijing, Julai 25.

Michezo mingine ya Man Utd itakua dhidi ya klabu ya Salford City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England, Julai 26 na baada ya hapo watapambana na Galatasaray mjini Gothenburg nchini Sweden Julai 30.

Majaliwa akagua Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae (Tiles)
Kituo cha Polisi Kapenguria Kenya Chavamiwa