Timu ya kikosi cha wapiga mbizi KMKM imesitisha zoezi zima la uokoaji katika bahari ya Hindi tangu kuzama kwa boti iliyosababisha vifo vya watu 10 waliokuwa wakielekea msibani
Kiongozi wa KMKM, Kasim Khalfan amethibitisha kuwa taarifa za sasa hazioneshi ushahidi wa watu waliopotea majini kwa kuwa siku ya kwanza miili kumi ilipatikana na watu kumi waliokolewa na siku ya pili timu ya uokoaji haikumpata mtu mwingine yeyote.
Aidha familia zilizopoteza wapendwa wao bado zinaendelea kuomboleza na miili yote kumi imezikwa tayari lakini taarifa za awali zinasema bito iliyozama ilikua imebeba watu zaidi ya 30.
Kwa mujibu wa walionusurika wanasema injini ilizima mara mbili kisha boti ikaanza kuzama.
Hata hivyo wananchi wa eneo hilo hawajafurahishwa na kitengo cha uokoaji cha KMKM kwa kuwa walichelewa kufika licha ya kituo chao kuwa karibu na watu wengi waliokolewa na wanakijiji wanaojua kuogelea katika eneo hilo.
Boti hiyo ilizama siku ya Jumanne ikiwa imebeba abiria wanaosemekana kuwa wa kiume tupu waliokuwa wakielekea kwenye mazishi ya ndugu yao na boti iliyokua imebeba mwili ilivuka salama ingawa ya abiria ndio ilizama.