Manchester United itawalazimu kusubiri hadi mwanzoni mwa mwezi ujao, ili kuhitimisha mpango wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic.

United wataruhusiwa kumsajili Ibrahimovic katika kipindi hicho, baada ya kubainika kwamba, mkataba wa mshambuliaji huyo na klabu ya Paris St-Germain unambana kufanya maamuzi ya kusaini sehemu nyingine, kwa kigezo cha kukusanya marupurupu ya mafao yake.

Mbali na Ibrahimovic, pia mkataba huo umemjumuisha wakala wake Mino Raiola ambaye anapaswa kupata sehemu ya mgao wa marupurupu hayo, na tayari baadhi ya vyombo vya habari vimetaja kiasi cha Pauni milion 4 kuwa stahiki yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alitarajiwa kumalizana na uongozi wa Man Utd hapo jana, lakini haikuwa hivyo kutokana na kuogopa kupoteza haki yake ya gawio la pesa kutoka PSG.

Hata hivyo tayari, mazunguzmo kati ya wakala wa Ibrahimovic na uongozi wa Man Utd yameshafanyika na utaratibu wa kuhamia Old Trafford utachukua nafasi yake kuanzia Juni 30.

Ibrahimovic amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Man Utd, na atakua akilipwa mshahara wa Pauni 275,000 kwa juma.

Mkataba huo pia una kipengele cha kuongezewa muda mwingine zaidi wa kuendelea kuwepo klabuni hapo, endapo kiwango chake kitamridhisga Jose Mourinho pamoja na jopo lake la ufundi.

Ronald Koeman Kuhamia Goodson Park
Video: Watumishi hewa wa bungeni kupoteza milioni 40 kwa siku