Aliyekuwa kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Déguy Alain Didier Zokora, ameelekea nchini India kumalizia soka lake kabla ya kutangaza kustaafu.

Kiungo huyo aliyewahi kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza amethibitisha kujiunga na klabu ya FC Pune City inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini India.

Zokora mwenye umri wa miaka 34, alithibitisha safari yake ya nchini India kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa kuamini kuwa ni njia rahisi kwake kuwafikishia ujumbe mashabiki pamoja na watu wake wa karibu.

Zokora, alitangaza kustahafu kutimikia timu ya taifa ya Ivory Coast mwaka mwaka 2014, baada ya kuwa sehemu ya kiksoi cha timu hiyo tangu mwaka 2000 huku akicheza michezo 123 na kufunga bao moja.

Klabu nyingine ambazo aliwahi kuzitumikia mbali na Spurs ya nchini England ni ASEC Mimosas ya nchini kwao Ivory Coast, Racing Genk ya nchini Ubelgiji, St Etienne ya nchini Ufaransa, Sevilla FC ya nchini Hispania, Trabzonspor na Akhisar Belediyespor, zote za nchini Uturuki.

Ndugai Adai Alipiga Simu Na Sio Mtu, Aliyeshambuliwa Atoa Ya Moyoni
Herve Renard Amvuta Tena Sunzu Ufaransa