Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila ametaja siri ya ushindi wake wa kwanza baada ya kurudi tena akitokea Ihefu FC kuwa ni kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake na huu ni mwanzo tu.

Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold, ukiwa ushindi wao wa kwanza kwenye mechi saba walizocheza wakifungwa mechi nne, sare mbili.

Katwila ambaye aliondoka miaka mitatu iliyopita kweye timu hiyo amesema hajakaa na timu kwa muda, alichokifanya ni kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake na anashukuru Mungu mbinu hizo zimembeba.

“Nimekabidhiwa timu ikiwa tayari imeanza maandalizi ya kuivaa Geita Gold nilichofanya baada ya kukaa na wachezaji ni kuwaambia kuwa hakuna kisichowezekana wanatakiwa kuwekeza nguvu na akili kwenye mchezo huo ili weweze kufikia lengo la kupata ushindi.

“Nashukuru Mungu mambo yakaenda kama tulivyopanga na wamenipa nguvu ya namna ya kuwapambania ili waweze kurudi kwenye ushindani kama ilivyokuwa misimu ya nyuma, nafikiri sasa ndiyo tumeanza na mengine mazuri yanakuja” amesema.

Katwila alisema ni mwanzo mzuri kwake na ametambua ubora na upungufu wa kikosi chake atakijenga kwa ushindani na kuwania nafasi nzuri kwenye msimamo.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya pili kutoka mwisho (15) baada ya kukusanya pointi nne kwenye mechi saba ikichapwa na Simba nyumbani 4-2, Coastal Union sare 1-1, Dodoma Jliji 1-1.

Singida Big Stars ilichapa bao 1-0, ikafungwa mabao 3-2 dhidi ya Tanzania Prisons na kupoteza 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Kaburu aahidi makubwa Simba SC
Robertinho akiri mapungufu safu ya ulinzi