Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa kulikuwa na njama za kutaka kumuua mara baada ya kuonyesha msimamo wake wa kiuchumi na marekebisho ya umiliki wa ardhi nchini humo.
Ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wanachama wa ANC mjini Phongolo, Kwa Zulu Natal, ambapo rais huyo amesema kuwa kulikuwa na mkakati wa kutaka kumuua alipotaka kuweka marekebisho ya kiuchumi na umiliki wa ardhi nchini humo.
“Niliwekewa sumu na ningefariki kwa sababu baadhi ya wafanyabiashara wa Afrika Kusini waliungana na kundi la Brics linaundwa na mataifa ya Brazil, Urusi, India, China, kupinga marekebisho ambayo nilitaka kuyaweka chini ya utawala wangu, huku wakisema nilikuwa na mpango wa kuharibu uchumi,”amesema Zuma
Aidha, katika hotuba hiyo hakumtaja aliyetaka kutekeleza azma hiyo lakini aliishia kusema kuwa ni mtu wake wa karibu, huku akiongeza kuwa kulikuwa na majaribio matatu ambayo yote hayakufanikiwa.
Hata hivyo, siku za hivi karibuni Rais huyo wa Afrika Kusini alikabiliwa na wakati mgumu mara baada ya spika wa bunge hilo kuruhusu wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani kufuatia misimamo yake na maamuzi ambayo amekuwa akiyachuku.