Mwanamuziki chipukizi kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva Abby Chams ametumbuiza kwenye moja ya maonyesho makubwa ya biashara ya umoja wa falme za kiarabu liitwalo Expro2020 Dubai, hafla iliyozinduliwa mapema Oktoba mosi, 2021.
Abby chams licha ya kuwa ndio kwanza ameianza rasmi safari yake ya kimuziki, amepata fursa hiyo adhimu ya kutoa burudani kwa wahudhuriaji wa hafla hiyo, jambo linaloashiria ukuaji wa kisanaa kwa msanii huyo kinda kwenye tasnia ya muziki nchini.
Hili sio kubwa pekee kutokea kwa Abby , Ikumbukwe takribani mwezi mmoja uliopita alipata nafasi ya kuonekana na kuchangia mada kwenye kipindi maarufu cha televisheni huko nchini Marekani ‘The Kelly Clarkson Show’ kama mmoja wa vijana chipukizi wenye kufanya mambo yenye mlengo chanya katika jamii.
Tamasha alilohudhuria abby chams huko Dubai, ni miongoni mwa maonyesho ya kimataifa yenye kuhusisha fursa kwa mataifa kukutana pamoja na kuonyesha technolojia mpya, bidhaa mbali mbali na kutanua wigo wa mahusiano ya kibiashara baina ya wajasiriamali nk.
Maonyesho hayo hufanyika kwa namna mbali mbali, yakiwa yamedumu kwa takribani karne mbili tangu kuanzishwa kwake.
Abby Chams kwasasa anafanya vizuri kwemye chati mbali mbali za muziki nchini na wimbo wake mpya ‘Tucheze’ wenye jumla ya watazamaji laki moja na elfu sabini na nane (178k) kwenye mtandao wa youtube.