Moto uliotokea katika Jimbo la New South Wales nchini Australia umedhibitiwa na maafisa wa kupambana na moto huku ukiwa umeshasababisha vifo vya watu 33 nchini humo.

Udhibiti huo umekuwa rahisi baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo juzi na kusaidia kuzima moto uliokuwa ukiteketeza maeneo ya Mashariki mwa Australia tangu Septemba 2019.

Tangu Septemba 2019 eneo la ukubwa wa hekta milioni 10 limeteketezwa na zaidi ya nyumba 2,500 zimeharibiwa.

Moto huo ulichochewa na kiangazi cha muda mrefu kilichoshuhudiwa nchini humo mwaka 2019 kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Chama cha Madaktari kuteta na Magufuli ukosefu wa ajira
Serikali yamsaka Nabii aliyetangaza kutibu virusi vya Corona

Comments

comments