Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa leo ndio ulikuwa mwisho wa Mbao FC kuizuia Yanga kupata matokeo kwenye dimba la CCM Kirumba lililopo jijini Mwanza baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya mchezo Zahera amekiri kuwa baada ya kufungwa bao dakika za mwisho kipindi cha kwanza, aliwaambia wachezaji wake kuwa wakumbuke leo ndio siku ya mwisho ya kufungwa na Mbao FC.

”Sikujisumbua wakati wa mapumziko kuwaambia wachezaji wangu mapungufu ya Mbao FC badala yake niliwaambia kila mchezaji aseme leo ni mwisho na wakalibeba hilo wakaenda kupata matokeo,”amesema Zahera.

Hata hivyo, baada ya ushindi wa leo, Yanga sasa imefikisha pointi 61 kwenye mechi 25 na kuendelea kujikita kileleni kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili.

Video: Bavicha wazungumzia kesi ya Mbowe
Rais Dkt. Shein aweka wazi msimamo wake kuhusu uchaguzi Zanzibar

Comments

comments