Waziri wa Uchukuzi wa Cameroon, Jean Ernest Massena Ngalle Bibehe, amethibitisha vifo vya watu 14 waliofariki katika ajali ya basi iliyotokea eneo la mashariki mwa nchi hiyo na kujerui watu 68.

Bibehe amesema jali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka kutokana na mwendokasi na kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Amesema, ajali hiyo ilitokea siku ya Jumanne (Mei 2, 2023), katika kijiji cha Lom, mkoani Adamaoua ambapo kati ya watu hao waliofariki mmoja ni mtoto wa miaka 10.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la kimataifa la afya – WHO, Cameroon ni moja ya mataifa barani Afrika yenye idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani.

Dodoma Jiji yakataa kuwa ngazi ya Ubingwa
Guardiola amrudisha Messi FC Barcelona