Serikali kupitia Ofisi ya Makamu na Taasisi za Umma itaendelea kuimarisha mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa biashara ya kaboni ikiwemo kuimarisha mifumo ya usajili wa makampuni ya uwekezaji wa biashara ya kaboni hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani amesema Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha kuwa jamii, na wadau mbalimbali wanaohusika na biashara hiyo ikiwa pamoja na inanufaika kikamilifu kutokana na faida zilizopo katika biashara ya kaboni nchini.

Kwa upande wake, Rais wa Shirika la ZGGEP Donovan Griay ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa hatua kubwa iliyofikia katika uendelezaji wa biashara ya kaboni nchini na kueleza utayari wa Shirika hilo kuja kuwekeza nchini kwa kuanzisha miradi ya biashara ya kiuchumi na kuibua fursa
kwa jamii.

“Tupo tayari kuwekeza na tumejipanga kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa biashara ya kaboni inaibua fursa ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi” amesema Griay huku ikikumbukwa kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, Itifaki ya Kyoto na Makubaliano ya Paris inayotekeleza Biashara ya Kaboni.

Kitumbo, Ulimboka wafungiwa maisha
Mawakili wasio waadilifu wawajibishe - Dkt. Mpango