Boniface Gideon – Tanga. 

Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Tanga kimewapiga jeki Vijana wanaojihusisha na Biashara ya kuuza Nyama na Mafundi Magari waliopo katika soko kuu la Mgandini kwa ajili ya kununua vitendea kazi vyao ikiwemo Mitambo ya kuchunguza tatizo la gari, kujaza upepo na Vifaa vya Michezo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kukagua na kuzindua Matawi ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahman amesema chama hicho kitahakikisha kinaisimamia Serikali ili Vijana wapate Mikopo ya Halmashauri.

Amesema, “tumekuja hapa sokoni kuona changamoto mlizonazo Vijana, mmesema mnahitaji Mitambo ya kuchunguza tatizo la gari pamoja na mtambo wa kujaza upepo na vifaa vya michezo,basi chama kimewasikia na tunawakabidhi fedha Sh.4,500,000 ili mpate kununua vitendea kazi kama mliomba.”

Aidha, Abdulrahman pia aliwataka Vijana kuacha tabia ya kukaa vijiweni bila kazi kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira na kusema, “Vijana fanyeni kazi kwa bidii acheni kukaa vijiweni, fanyeni kazi, ukifanya kazi Mungu naye anakufungulia milango ya kipato na kuongeza maarifa zaidi, Chama kitaendelea kuisimamia Serikali hususani kwenye utoaji wa Mikopo ya Halmashauri kuanzia mwezi wa Saba.”

Wakati huohuo Chama hicho kimeibomoa Ngome za Chama cha Demokrasia na Maendeleo  – CHADEMA, Mkoa wa Tanga baada yaViongozi  watatu wa ngazi za juu katika chama hicho akiwemo Aliyekuwa Diwani wa Viti maalumu Wilaya ya Muheza Ashura Kachenje ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Muheza (BAWACHA).

Wengine ni Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tanga ambaye aliratibu Maandamano ya Amani wiki iliyopita, pamoja na Katibu wa BAWACHA Wilaya ya Tanga.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 7, 2024
Silaha, Pikipiki zaidi ya 100 zadakwa, watatu mbaroni