Lydia Mollel – Morogoro.

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu watatu, wawili kati yao wakidaiwa kuhusika na wizi wa Pikipiki Wilayani Kilosa na huku mmoja akikamatwa na Silaha aina ya Gobole ambapo katika operesheni hiyo zaidi ya Pikipiki 100 zimekamatwa.

Akizungumza na Dar 24 Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema watuhumiwa hao ni Edson Msowela (27), Mkulima na mkazi wa Mvumi aliyekamatwa na Pikipiki yenye namba za usajili MC 710 EFK aina na Haoujue.

 

Mwingine ni Ally Waziri (30), Mfanyabiashara mkazi wa Dumila aliyekamatwa na Pikipiki namba za usajili MC 442 EEL aina ya Haojue na Shaban Shamte (30), aliyekamatwa akiwa na Silaha aina ya Gobole ambayo anadaiwa kuitumia kufanya uhalifu.

Kamanda Mkama amesema katika oparesheni za Jeshi hilo ambapo zaidi ya pikipiki 100 zilizokuwa zikijihusisha na uhalifu Mkoani hapo zimekamatwa na uchunguzi unaendelea ili kuwafikishwa watuhumiwa Mahakamani.

Wauza Nyama, mafundi wa Magari wapigwa jeki Tanga
Kitwanga: Tukiamua kubadilika Polisi watabadilika