Mlima Kilimanjaro ulio mrefu zaidi barani Afrika unawaka moto, sababu ya moto huo unaowaka umbali wa mamia ya mita kutoka usawa wa bahari bado hazijajuikana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa nahifadhi ya taifa ya Kilimanjaro (KINAPA), moto huo ulitokea jioni ya jana Jumapili jioni.
Mashuhuda wamesema kuwa jitihada za wakazi kuuzima moto huo zinaendelea lakini changamoto inayokumba zoezi hilo ni umbali ambao moto huo upo.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWMSO) amewaomba Wanafunzi waliopo Chuoni kushiriki kikamilifu kuzima moto huo.
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa imesema sehemu ya msitu wa Mlima Kilimanjaro ilianza kuungua tangu jana mchana, na wanaendelea na jitihada za kuuzima
Afisa habari wa Shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA)Patrick Shelutete amethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa taarifa kwa kina kuhusu tukio hilo itatolewa.