Mgombea udiwani wa kata ya Mzimuni Wilaya ya Kinondoni Manfred Lyoto kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema, vijana wanaoishi katika jiji la Dar es Salaam hasa wa kata hiyo watarajie kupata ajira mara tu baada ya Uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020 kumalizika.

Ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema swala la ajira katika kata ya Mzimuni tayari lina mbadala wake.

Hata hivyo amesema, mbali na changamoto  ya vijana kutokuwa na ajira lakini pia zipo changamoto mbalimbali ambazo wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakikumbana nazo ambapo, amesema ikiwa atapewa ridhaa ya kuongoza atahakikisha anazishughurikia  tena kwa haraka.

”Ninatambua kuwepo kwa changamoto nyingi kubwa ni baadhi ya barabara zetu kutopitika nipende kuahidi kwamba hili nalo nitalishughulikia pamoja na nyingine nyingi;”amesema Lyoto.

Aidha amewaomba wananchi kumchagua na kumpa nafasi ya kuwa diwani wa kata hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 ambapo amesema atatatua changamoto zilizopo katika kata hiyo.

Serikali kujenga 'Flyover' 11 kwa miaka mitano
Moto wawaka Mlima Kilimanjaro, jitihada za kuuzima zaendelea