Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa rais kwa muhula wa pili, serikali yake itajenga barabara za juu (flyover,) zaidi ya 11 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Magufuli amesema hayo leo Oktoba 12 wakati akiwahutubia wananchi wa jimbo la Segerea wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa Kinyerezi.

“Na katika kipindi cha miaka mitano inayokuja tunajenga flyover zaidi ya 11 katika jiji la Dar es Salaam, Dar rs Salaam litakuwa jiji kama Ulaya, na tutawazidi hata nchi nyingine za Ulaya,” amesema Magufuli.

Aidha, amesema Ujenzi wa mradi wa usambazaji maji unaoendelea eneo la Pugu wilaya ya Ilala unatarajiwa kumalizika Disemba mwaka huu.

Kwa upande mgombea ubunge wa jimbo la Ilala Musa Azan Zungu amewataka vijana kutokubali kutumikishwa kwa kuingia kwenye maandamano bali waendelee kudumisha amani ya nchi.

Mgombea huyo ataendelea na kampeni kesho Oktoba 13 ambapo atakuwa katika viwanja vya Mburahati wilaya ya Ubungo.

Kim azindua silaha nzito za kivita
Changamoto ya kutokuwa na ajira itaisha - Lyoto