Siku moja baada ya Korea Kaskazini kuandaa mkutano mkubwa wa kuadhimisha miaka 75 ya chama cha wafanyakazi nchini humo na kuonesha silaha mpya kubwa, Korea Kusini imefanya kikao cha dharura na kutoa taarifa ya kuikumbusha Korea Kaskazini kuhusu makubaliano yao ya kuzuia mapigano.

Ofisi ya Rais ya Korea Kusini, imesema kuwa makubaliano ya kuzuia mashambulizi ya silaha kati ya Mataifa hayo mawili ya Korea lazima yaheshimiwe.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa wito wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili pindi janga la Corona litakapoisha na kutumia fursa hiyo kuzindua silaha mpya kubwa ambayo waangalizi wanaamini ni Kombora la Masafa Marefu lenye uwezo wa kutoka Bara moja kwenda Bara lingine.

Jeffrey Lewis, Profesa katika Taasisi ya mitaala ya Kimataifa ya Middlebury amesema ni dhahiri kwamba kombora hilo linalenga kudhoofisha mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani katika Jimbo la Alaska.

Mafunzo kazini kuimarisha utendaji kazi wa vijana
Serikali kujenga 'Flyover' 11 kwa miaka mitano