Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wamewataka waajiri nchini kuendelea kutoa nafasi na mafunzo katika maeneo ya kazi pamoja na kuanzisha kwa mafunzo ya uanagenzi ili kutengeneza ajira .

Hayo yamesemwa na Mkurugengnzi Mtendaji wa ATE Dkt.Aggrey Mlimuka kwenye kampeni ya kuhamasisha programu ya uanagenzi kwa waajiri inatajwa kuongeza uelewa kuhusu mafunzo ya ujuzi mahala pa kazi ikiwemo kuchukua wahitimu wa vyuo ili kuwajengea uzoefu wa kazi katika kampuni.

“Tumekuwa  tukisisitiza waajiri kuendelea na utaratibu wa kupokea vijana kwanza wanasaidia makampuni kupunguza gharama za uendeshaji lakini pia kutengeneza watu wenye ujuzi,”.

Aidha, amesema mpango wa serikali wa awamu ya pili wa maendeleo unasisitiza zaidi ya uwepo wa watu wenye ujuzi na kwamba ATE imekuwa ikisisitiza kwa muda wote wa miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1960, huku ikiendelea kuwakilisha maslahi ya waajiri kwenye mijadala yote ya kitaifa.

Uendelezaji ujuzi kwa vijana ni moja ya kipaumbele kilichopo katika dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.

Maalim: "Kiwango cha mshahara kitakuwa laki 5"
Kim azindua silaha nzito za kivita