Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo amesema lugha ya Kiswahili ni fursa na inatakiwa itumiwe kukuza uchumi kwani kimekubalika na kuzungumzwa katika mataifa mbalimbali duniani.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wadau wa Kiswahili, Wasanii na Wanafunzi kwenye Tamasha la Hamasa ya Shamrashamra ya Swahili festival, lililofanyika katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam ambapo.

Amesema “nimeona kuna fursa nyingine tunazo lakini hatuzioni au hatuzitumii tutumie fursa ya Kiswahili , mswahili na tamaduni zake, chakula chake,Sanaa yake, kivazi chake, manukato yake na maisha yake kwasababu huo ndio utambulisho wenu nyinyi nyote”

Amesema “lugha ya Kiswahili imekuwa na kutambulika ni lugha rasmi ya kimataifa na Shirika la elimu sayansi utamaduni duniani UNESCO Sasa ni juu yetu kukipa kipaumbele kwa kuweka kiswahili chetu bendera juu maana tusipoweka sisi kitawekwa na mataifa mengine kwasababu ni fursa hiyo.”

Balozi Kombo ameongeza kuwa, “na fursa ikitokea lazima uitumie kwani goli likiwa wazi usipofunga wewe watafunga wengine kwani kiswahili kinazungumzwa na kimekubaliwa kimataifa na nchi zaidi ya 30 ambapo nchi ya kwanza ni Tanzania ya pili Kenya, ya tatu Uganda, ya nne Rwanda, tano Burundi, sita Congo, saba Sudani ya kusini nane ni nchi za SADAC.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Women Ubuntu Tanzania, Dkt. Angella Gloria Bondo amesema wanahamasisha siku ya Tamasha la Kiswahili duniani Julai 7 kama ambavyo UNESCO walivyotoa azimio hilo mwaka 2021.

Amesema, “tunachofanya sisi ni kuhamasisha kwamba siku hii inakuja na imeandaliwa huko nchini Italia ili kwamba na Watanzania waliopo kule wapate fursa ya kuona kuna jambo kubwa ambalo limendaliwa na ubalozi pamoja na Asas hiyo”

Naye Afisa Elimu Kijiji cha Makumbusho Helmina Joseph amesema unapozumza lugha ya Kiswahili unazungumzia utamaduni wa mtanzania na kwamba Tanzania ina bahati kwani kuna makabila 120 ambayo yote yanazungumza lugha ya Kiswahili inayowatambulisha na kuwaunganisha.

Kikeke: Vijana pambanieni ndoto zenye malengo
Kocha Dodoma Jiji anaitaka Ligi Kuu